1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Harris amshambulia Trump na kumtaja kama tishio kwa wanawake

21 Septemba 2024

Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris amemshambulia Donald Trump na kumtaja kama tishio kwa uhuru wa wanawake.

USA, Philadelphia | Trump-Harris Presidentschafts-Debatte
Makamu wa rais wa Marekani Kamala HarrisPicha: Brian Snyder/REUTERS

Katika hotuba aliyoitoa katika jimbo la Georgia jana Ijumaa, mgombea huyo wa urais wa chama cha Democratic amesema Donald Trump ataondoa ruhusa ya utoaji mimba iwapo atachaguliwa kuwa rais.

Ameyasema hayo siku chache tu baada ya shirika la habari la uchunguzi la ProPublica kuripoti kuwa wanawake wawili katika jimbo hilo walikufa baada ya kukosa matibabu sahihi kwa matatizo ya kiafya yaliyojitokeza baada ya kumeza tembe za kuavya mimba.

Soma pia:  FBI yasema Trump alilengwa katika jaribio la mauaji

Kulingana na utafiti wa kura ya maoni kuelekea uchaguzi wa urais, takriban wapiga kura sita wanawake kati ya kumi wanamuamini Kamala Harris zaidi ya Donald Trump linapokuja suala la utoaji mimba, huku takriban wanawake wawili kati ya kumi wakimuamini Trump.

Nusu ya wapiga kura wanaume wanamuamini Harris kuliko Trump kuhusu utoaji mimba, huku takriban theluthi moja wakimuamini Trump kuliko Harris.