Marekani yatangaza mipango ya kukuza biashara na Tanzania
30 Machi 2023Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Ikulu ya Dar es Salaam, Harris amesema miongoni mwa yaliyofikiwa ni kupatikana hati mpya ya makubaliano kati ya Benki ya Mitaji ya Marekani ya EXIM na serikali ya Tanzania.
Mpango huo utawezesha ufadhili wa hadi dola milioni 500 katika kusaidia makampuni ya Marekani kuuza biadhaa na huduma nchini Tanzania katika sekta za miundo mbinu, usafiri, teknolojia ya kidijitali, tabia nchi na upatikanaji wa nishati pamoja na uzalishaji umeme.
Kamala aanza ziara ya siku tatu nchini Tanzania
Aidha, makamu huyo wa rais amekaribisha hatua zinazochukuliwa na serikali ya Tanzania katika kujenga ustawi bora wa kidemokrasia.
Amesema Tanzania imechukua mkondo mpya unaotoa matumaini yanayoonyesha ni kwa kiasi gani matakwa ya kuheshimu demokrasia ya raia inavyopaswa kuzingatiwa.