1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamala Harris kumtangaza mgombea mwenza

5 Agosti 2024

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris, anatarajiwa kumtangaza mgombea mwenza wake kesho Jumanne.

Kamala Harris
Makamu wa Rais wa Marekani anayetazamiwa kuwa mgombea urais kupitia Democrat, Kamala Harris.Picha: Aaron Schwartz/CNP/picture alliance

Kulingana na vyanzo vinavyofahamu taarifa hiyo, Kamala aliwahoji wagombea kadhaa wa nafasi hiyo katika makaazi yake mjini Washington mwishoni mwa wiki. 

Uamuzi wa ni nani atakayemteua kuwa mgombea mwenza unatarajiwa kutolewa kesho mjini Philadelphia, kabla ya wawili hao kuelekeza kampeni zao katika majimbo yenye ushindani mkali.

Soma zaidi: Trump: Nipo tayari kwa mdahalo na Harris Septemba 4

Wagombea wakuu watatu waliohojiwa katika nafasi hiyo ni gavana wa Minnesota, Tim Walz, Seneta wa Arizona, Mark Kelly, na gavana wa Pennsylvania, Josh Shapiro.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW