1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLebanon

Kamanda wa Hezbollah auawa katika shambulizi la anga

17 Agosti 2024

Jeshi la Israel limesema limemuua hivi leo kamanda wa kundi la wanamgambo la Hezbollah katika shambulio la anga kusini mwa Lebanon. Mwanamume huyo aliuawa karibu na mji wa pwani wa Tiro.

Shambulizi la Israel katika eneo la Khiam kusini mwa Lebanon mnamo Agosti 6,2024
Shambulizi la Israel katika eneo la Khiam kusini mwa LebanonPicha: Ramiz Dallah/Anadolu/picture alliance

Awali, wizara ya afya ya Lebanon ilitangaza kwamba mtu mmoja aliuawa katika shambulizi la Israel lililolenga pikipiki katika eneo hilo.

Jeshi la Israellimesema aliyeuawa alikuwa kamanda wa kikosi cha Radwan, kitengo cha wasomi ndani ya kundi hilo la Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran. Kundi hilo halikutoa tamko lolote juu ya shambulizi hilo wala madai ya Israel.

Soma pia:Watu 10 wauawa katika shambulizi la bomu kusini mwa Lebanon

Mara kwa mara, Hezbollah imekuwa ikirusha roketi kutoka kusini mwa Lebanon hadi kaskazini mwa Israel tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Palestina la Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Jeshi la Israel limejibu kwa mashambulizi mengi ya anga pamoja na mashambulizi ya makombora na  kuyalenga maeneo ya kusini mwa Lebanon.