1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Kamanda wa Kikurdi atangaza usitishaji vita Syria

11 Desemba 2024

Kamanda wa kikosi cha wapiganaji wa Kikurdi Syria ametangaza makubaliano yaliyosimamiwa na Marekani ya usitishaji vita Kaskazini mashariki mwa Syria

Kamanda wa kikosi cha SDF Mazloum Abdi
Kamanda wa kikosi cha SDF Mazloum AbdiPicha: Baderkhan Ahmad/AP Photo/picture alliance

Kamanda wa kikosi cha wapiganaji wa Kikurdi kinachodhibiti eneo kubwa la Kaskazini Mashariki mwa Syria, amesema wamefikia makubaliano ya kusitisha vita katika eneo linalokaliwa na jamii kubwa ya waarabu la Manbji.

Kamanda wa kikosi cha SDF Mazloum Abdi amesema makubaliano hayo yamefikiwa na wapiganaji wanaoungwa mkono na Uturuki, chini ya usimamizi wa Marekani na kuongeza kwamba wapiganaji wa kikosi cha SDF wataondolewa kwenye eneo hilo la Manbji hivi karibuni.

Makubaliano hayo yametangazwa leo baada ya hapo jana kutangazwa kwa  kiongozi mpya wa serikali ya mpito ya Syria, Mohammed al Bashir ambaye amewatolea mwito wasyria waliokimbilia nje warejee nyumbani.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ameitaka serikali hiyo mpya kutimiza ahadi zake za kuheshimu kikamilifu haki za walio wachache na kutowa msaada wa kiutu kwa watu wote wenye uhitaji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW