1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamati ya bunge Kenya yataka mageuzi tume ya uchaguzi

Iddi Ssessanga Thelma Mwadzaya
27 Novemba 2023

Kamati ya bunge la Kenya imetoa wito wa mageuzi ya tume ya uchaguzi na kupita upya kwa sera ya kodi, matumizi ya umma na ustawi wa jamii, katika ripoti yake iliyolenga kushughulikia malalamiko ya muungano wa upinzani.

Wahlen in Kenia I William Ruto
Picha: Thomas Mukoya /REUTERS

Kamati hiyo inayoundwa na wajumbe kutoka mirengo yote ya kisiasa ili kupitia malalamiko ya upinzani inataka kuundwa upya kwa tume ya uchaguzi na kufanyika ukaguzi wa matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwaka uliyopita.

Hata hivyo ripoti ya kamati hiyo, maarufu kama NADCO, imezua hisia mseto ndani na nje ya serikali kuu, huku rais Ruto akiahidi kutekeleza mapendekezo yaliyo ndani ya uwezo wake, na viongozi wengine ndani ya muungano wake na wale wa upinzani wakiipinga.

Kenya ilikumbwa na maandamano ya vurugu mapema mwaka huu yaliosababishwa na malalamiko ya viongozi wa upinzani na wafuasi wao kuhusu udanganyifu katika uchaguzi, gharama kubwa za maisha na kodizinazoogezeka.

Kama matokeo, kamati hiyo iliundwa mwezi Agosti kwa uungwaji mkono wa azimio la bunge na ilipewa mamlaka kuchunguza malalamiko hayo na kupendekeza mageuzi muhimu kwa serikali.

Kamati ya maridhiano imependekeza tume ya uchaguzi ifanyiwe mageuzi ili kuifanya kuwa huru zaidi.Picha: Brian Inganga/AP Photo/picture alliance

Mabadiliko ya muunda wa Tume huru ya Uchaguzi

Katika ripoti yake, kamati ilipendekeza mabadiliko na muundo mpya wa tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC, ambayo inashughulikia masuala ya uchaguzi.

Soma pia: Wasiwasi wa kurejea kwa kundi la Mungiki

"Kamati inapendekeza uteuzi wa jopo la wataalamu ambao watatathmini mchakato wa uchaguzi wa 2022 na mfumo wa kutathmini chaguzi za baadae." Ripoti hiyo ilichapishwa siku ya Jumamosi.

Serikali, ilisema kamati hiyo katika ripoti, inapaswa kupitia upya sera yake ya kodi, kupunguza matumizi ya umma na kutanua ulinzi wa kijamii.

Rais wa sasa William Ruto alichaguliwa Agosti mwaka jana kwa ahadi ya kuwasaidia wafanyakazi maskini wa Kenya, lakini wakosoaji wanasema badala yake ametekeleza sera za kodi zinazidisha makali kwa Wakenya wa kawaida ambao tayari wanapambana kumudu mahitaji ya msingi.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, ambaye alishindwa na Ruto katika uchaguzi wa 2022, alikataa matokeo ya kura hiyo na anasema ushindi wake uliporwa.

Kenya imekumbwa na maandamano ya machafuko kupinga matokeo ya uchaguzi na gharama kubwa za maisha.Picha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Amekuwa akidai kupitiwa upya kwa matokeo ya uchaguzi na mageuzi mengine makubwa yakiwemo kufumuliwa kwa tume ya IEBC ili kuifanya huru zaidi.

Soma pia: Rais Ruto atangaza mikakati ya kukabiliana na mafuriko

Katika ripoti yake, kamati hiyo pia ilipendekeza "kuundwa na kuimarisha ofisi ya waziri mkuu katika katiba kama njia ya kuboresha utawala na uratibu wa majukumu ya mhimili wa utendaji serikalini.

Katika ujumbe wa mtandao wa kijamii wa X, msemaji wa ikulu ya Kenya Hussein Mohamed alisema Ruto amejitolea kutekelea mapendekezo ya kamati hiyo.

Kenya yaanza mchakato wa kukusanya sahihi kufanyia katiba mageuzi

02:58

This browser does not support the video element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW