1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamati ya kifo cha Garang yaanza uchunguzi

14 Agosti 2005

Khartoum:

Kamati ya taifa ya Sudan iliyoteuliwa kuchunguza kifo cha Makamu wa kwanza wa Rais na aliyekuwa Kiongozi wa Waasi, hayati John Garang, itaanza kazi leo. Mjumbe wa Kamati, Siraj Eddin Hamid, amesema kuwa Kamati itafanya mawasiliano ya kina ndani na nje ya Sudan ili kupata habari zitakazosaidia kufahamu sababu zilizosababisha ndege hiyo kuanguka. Rais Omar al-Bashir wa Sudan ametangaza Agosti nane kuteuliwa kwa Kamati yenye Wajumbe saba inayoongozwa na aliyekuwa Makamu wa Rais Abel Alier. Garang amefariki Julai 30 wakati helikopta ya Rais Museveni wa Uganda aliyokuwa akisafiria kutoka Uganda hadi kusini mwa Sudan ilipoanguka. Kifo chake kimesababisha machafuko na watu kuuawa mjini Khartoum na kusini mwa Sudan na baadhi ya Wasudan wa kusini wakidai kuwa serikali inahusika na kifo chake. Rais Museveni wa Uganda amesema kuwa kuanguka kwa ndege hiyo, ambapo hapo awali imekuwa ikidaiwa kuwa ni kwa sababu ya hali mbaya ya hewa, huenda ikawa siyo ajali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW