SiasaMarekani
Trump huenda akateuliwa mgombea 'asiye rasmi' wa Republican
26 Januari 2024Matangazo
Haya yanatokea ingawa ni majimbo mawili pekee yaliopiga kura, huku Trump akiwa mbali na idadi ya wajumbe inayohitajika kujipatia nafasi hiyo.
Hii ni kulingana na rasimu iliyoonekana jana na shirika la habari la AP.
Kuidhinishwa kwa Trump kutampa udhibiti zaidi wa chama cha Republican
Ikiwa Trump ataidhinishwa, hatua hiyo itaimarisha zaidi udhibiti wake kwa chama hicho na uendeshaji wa shughuli zake wakati ambapo balozi wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley bado yuko katika kinyang'anyiro cha uteuzi huo wa chama.
Soma pia:Trump akaribia uteuzi wa chama chake huko New Hampshire
Mwenyekiti wa kamati hiyo ya kitaifa ya chama cha Republican Ronna McDaniel tayari ameashiria kuunga mkono hatua hiyo.