1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoItaly

CERD yaelezea wasiwasi kuhusu soka ya Italia

1 Septemba 2023

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kukabiliana na Ubaguzi wa Rangi (CERD) imeelezea wasiwasi kuhusu soka ya Italia katika matokeo ya uchunguzi wake yaliochapishwa siku ya Alhamisi.

Wachezaji wa AS Roma na kocha wao Jose Mourinho wakiwasalimia mashabiki katika uwanja wa Olimpico mjini Rome nchini Italia mnamo Mei 6, 2023
Wachezaji wa AS Roma na kocha wao Jose Mourinho wakiwasalimia mashabikiPicha: Andrea Staccioli/Insidefoto/IMAGO

Katika taarifa, CERD imesema kuwa kuhusu Italia, imetiwa hofu na wanasiasa na maafisa wa ngazi za juu wa serikali wanaotumia matamshi ya chuki na mijadala ya kisiasa ya kibaguzi dhidi ya makabila madogo hasa Waroma, Wasinti na Camminanti, Waafrika na watu wa asili ya Kiafrika.

CERD yaelezea wasiwasi kuhusu ubaguzi katika michezo

Kamati hiyo pia imeelezea wasiwasi kuhusu visa vya ubaguzi wakati wa hafla za michezo vinavyojumuisha mashambulizi ya kimwili na maneno dhidi ya wanariadha wa asili ya Kiafrika.

CERD yataka waliohusika na ubaguzi  kuwajibishwa

CERD, imeitaka Italia kuchunguza dhuluma zote za kibaguzi katika michezo na kuwawajibisha waliohusika.

Mwanachama mmoja wa kamati hiyo, Regine Esseneme, raia wa Cameroon, ameihimiza Italia kuzingatia kwa makini visa hivyo vya ubaguzi vinavyozidi kuongezeka dhidi ya watu weusi na watu wa asili ya Kiafrika.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW