1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kambi ya amani Israel na Palestina yatikishwa na vita Gaza

Saleh Mwanamilongo
22 Novemba 2023

Kambi ya amani ya Israel na Palestina kwa muda mrefu imekuwa ikiendeleza mazungumzo dhidi ya chuki na umwagaji damu, lakini shauku iliyochochewa na vita vibaya zaidi vya Gaza bado inaleta changamoto.

Waandamanaji wanaounga mkono kusitishwa mashambulizi ya Israel Gaza
Waandamanaji wanaounga mkono kusitishwa mashambulizi ya Israel GazaPicha: Annette Riedl/dpa/picture alliance

Wengi wa wanaharakati wa Kambi ya amani wanaamini kwamba kuzungumza na kila upande kwa sasa ni muhimu zaidi kuliko hapo awali, wakati ambapo mapigano yanapamba moto na pande zote mbili zinaomboleza maafa yao.

Sulaiman Khatib wa shirika la Fighters for Peace, au Wapiganaji kwa ajili ya Amani, kundi alilolianzisha mwaka 2006 na ambalo wanachama wake wa Israel na Palestina hufanya mikutano ya kila wiki na maandamano ya mara kwa mara, amesema haikuwa rahisi kabla ya vita. Lakini sasa ni vigumu zaidi kuanzisha uhusiano na kila mmoja huko Israeli na Palestina ambapo misimimo mikali imeongezeka.

Vita vya Gaza vimeleta mateso yasiyo ya kawaida kuliko hata wakati wa viwango vya juu vya mzozo wa miongo kadhaa ambao umesababisha machafuko mara mbili ya Wapalestina na vita vinne vya hapo awali vya Gaza.

Oktoba 7, wanamgambo wa Hamas huko Gaza walishambulia Kusini mwa Israeli na kuua watu 1,200 na kuwashikilia mateka 240.

Soma pia:Umoja wa Mataifa umesifu makubaliano kati ya Israel na Hamas ya kuwaachilia mateka na kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.

Israel ilijibu shambulizi hilo kwa kuanzisha mashambulizi makali ya anga na ardhini ambayo yameharibu maeneo makubwa ya Gaza na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 13,000 kwa mujibu wa serikali ya Hamas, huku wakazi wake milioni 2.4 wakistahimili adhabu ya kuzingirwa.

Jioni moja ya hivi karibuni, kikundi kidogo cha wanaharakati wapatao 40 wa Israel na Palestina walikusanyika kando ya kuta za Mji Mkongwe wa Jerusalem kukaa kimya kwa dakika 15 kuwakumbuka waliopoteza maisha yaokatika mzozo wa sasa.

Wakiwa wamesimama na macho yao yakiwa yamefumba au kulia, walisikiliza ibada za Kiyahudi na za Kikristo chini ya uangalizi wa wapita njia.

Kambi ya amani ilikuwa ni jibu dhidi ya chuki?

Kambi ya amani daima imekuwa ikiwafanya baadhi ya watu kutembelea pande zote mbili. Lakini bado kambi hiyo inajumuisha zaidi ya mashirika 200, mengine yakiwa na zaidi ya miaka 40 toka kuundwa kwake.

Waandamanaji Ujerumani wakionesha mshakamano na PalestinaPicha: Sean Gallup/Getty Images

Miongoni mwa wanaharakati hao ni wanamazingira kwa ajili ya amani, madereva wa magari wanaoendesha Wapalestina kuwatembelea madaktari nchini Israel, na kwaya za pamoja za Israel na Palestina.

Wanasalia kuamini kwamba wamekuwa sahihi kutetea mazungumzo. Kundi moja wapo linalojiita , Duru ya Wazazi, linaundwa na familia za Waisraeli na Wapalestina waliopoteza watoto wao kutokana na mzozo huo.

Yuval Rahamin, Mkurugenzi mwenza wa kambi ya amani anasematayari anaona watu ambao wanaweza kuja na kujiunga nao baada ya ghasia nyingi zilizotokea na itakuwa sehemu ya mchakato wa kibinafsi kwa baadhi yao.

Wanaharakati wengi, ambao hapo awali waliathirika kutokana na mashambulizi ya Oktoba 7, walianza tena mikutano yao ya majadiliano siku chache baadaye.

Soma pia:Israel na Hamas wafikia makubaliano ya kubadilishana mateka

Haijawa rahisi, wanasema, na sio tu kwa sababu ya changamoto za kiufundi kama vile vizuizi vya ziada vya barabarani katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.

Avner Wishnitzer, mwanzilishi mwenza wa shirika la Fighters for Peace amesema haijawahi kuwa ngumu kiasi hicho kusikia maoni ya mwingine. Katika hali ya sasa ya mazingira ya vita, alisema, pande zote zimevunjwa moyo na maumivu na hofu.

Maumivu ya Oktoba 7 yanazidi kuwa makali zaidi kwa baadhi kwa sababu wanaharakati wa amani walikuwa miongoni mwa waathiriwa.

Mmoja wao alikuwa Vivian Silver, mwanzilishi wa shirika la Women Wage Peace, ambaye aliuwawa huko Kibbutz Beeri.

Khatib alikiri kuwa vuguvugu hilo limetikiswa vibaya na kwamba wanaharakati wengi wanatatizika kwa hisia mchanganyiko na za kutatanisha.

Muungano wa Amani ya Mashariki ya Kati una zaidi ya vikundi 160 wanachama.

Mzozo wa Mashariki ya Kati wakaribia mwezi mmoja

01:17

This browser does not support the video element.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW