1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kambi ya kampeni ya Kamala kuelekea uchaguzi ujao

Josephat Charo
6 Agosti 2024

Kamala Harris anajiandaa kwa kampeni za uchaguzi wa rais Novemba 5, yapo yanayoendelea ndani ya kambi yake ya kampeni. Makamu huyo wa rais wa Marekani anajihusisha na kundi la washawishi wenye uwezo wa kusuka ajenda.

Marekani | Siasa | Kamala Harris na  Joe Biden
Makamu wa Rais na mgombea urais Marekani Kamala Harris akimlaki Rais Joe Biden.Picha: Matt Kelley/AP Photo/picture alliance

Seneta wa Marekani Laphonza Butler wa jimbo la California, alikuwa na jibu la kubeza wiki iliyopita alipoulizwa na MSNBC kuhusu uwezekano wa kukabiliwa na wimbi la mashambulizi ya kibaguzi na jinsia. Laphonza alisema yaleteni kwa sababu sisi sio wageni kwa mambo haya.

Kundi hilo la washauri ni watiifu sana kwa Harris na wanaipenda taaluma yake, wengi wao wakiwa walianza kumshauri tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa seneta mwaka 2017, kwa mujibu wa mahojiano yaliyofanyiwa watu wanne miongoni mwao na shirika la habari la Reuters, ambao wana uelewa wa watu walio karibu na wandani wa Harris.

Baadhi yao katika kundi hilo walimshawishi rais Joe Biden amteue mwanamke Mmarekani mweusi, na hasa Harris, kama mgombea wake mwenza katika uchaguzi wa 2020, katika wakati ambapo alikuwa ameahidi hadharani angemteua tu mwanamke katika nafasi hiyo.

Watu wa karibu wa Harris wanawajumuisha washauri na washirika kama vile Minyon Moore, mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya mkutano mkuu wa chama cha Democratic, DNC, mwenyekiti mwenza anayesimamia sheria za mkutano mkuu wa chama, Leah Daughtry, mwanachama wa kamati ya mkutano mkuu wa chama cha Democratic, Donna Brazile na Tina Flournoy, mkuu wa wawafanyakazi wa zamani wa Harris.

Soma pia:Kamala Harris kumtangaza mgombea mwenza

Hawa si wageni katika suala la utawala, huku wengi wao wakiwa na uzoefu wa kuhudumu katika utawala wa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton kati ya 1993 na 2001.

Harris, huenda akahitaji msaada wote anaoweza kuupata, ingawa kampeni yake imeanza vyema kwa nguvu. Harris anabaki kuwa kiongozi ambaye hajajaribiwa katika ngazi ya kitaifa, licha ya kuwa seneta wa zamani kutoka kwa jimbo lenye idadi kubwa ya wakazi la Marekani, California.

Alijitoa katika uchaguzi wa awali wa chama cha Democratic mnamo 2020 na yuko nyuma ya mgombea wa chama cha Republican Donald Trump katika baadhi ya majimbo yenye ushawishi mkubwa na mashindano makali katika mbio za urais za mwaka huu, kwa mujibu wa matokeo ya kura za maoni.

Majukumu muhimu kwa watu wake wa karibu

Kuna dalili za Harris kuondokana na mambo aliyokuwa akiyafanya miaka ya nyuma katika eneo moja. Kufikia sasa katika mwaka huu, baadhi ya watu wa familia yake, kwa muda mrefu kuliko washauri wake wa karibu, wamekuwa na jukumu muhimu kuliko ilivyokuwa katika uchaguzi wa 2020.

Dada yake mdogo Maya Harris, aliyesimamia kampeni fupi ya Kamala, hajaonekana katika nyakati muhimu msimu huu wa kampeni, kwa mujibu wa watu watatu walio karibu na timu ya kampeni ya Harris.

Washauri na watu wa familia waliojumuishwa katika ilani yake ima walikataa kutoa kauli yoyote ama hawakusema lolote walipoombwa kutoa maoni yao. Kampeni ya Harris haikusema chochote.

Je Kamala anaweza kumshinda Trump katika uchaguzi 2024?

01:58

This browser does not support the video element.

Harris, mwenye umri wa miaka 59, anakabiliwa na kinyang'anyiro kikali ana anahitaji kujiandaa kwa wimbi la mashambulizi kama alivyosema mshauri wa kimkakati wa chama cha Democratic, Anthony Coley.

Soma pia:Trump: Nipo tayari kwa mdahalo na Harris Septemba 4

Trump amemuita Harris kama mwendawazimu, mtu asiyejua lolote kama jiwe na kuhoji utambulisho wake kwa kupendekeza alikuwa awali amepuuza asili yake kama Mmarekani mweusi.

Baadhi ya wanachama wa chama cha Republican katika bunge la Marekani wanamdharau Harris kama mtu mwenye asili mchanganyiko aliyekodiwa afanye kazi. Wanaharakati wa mrengo wa kulia wamechafua kurasa zake mtandaoni kwa kauli za ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa kijinsia.

Coley anasema watu wa karibu na Harris wameshajaribiwa na kupata uzoefu katika hali itakayokuwa ya msaada katika siku zaidi ya 90 zilizosalia kuelekea uchaguzi wa Novemba 5.

Watafanya kazi kwa kasi, kwa bidii na kwa undani na ni muhimu kuwa na watu wanaojua njia ya kujibu haraka na kwa werevu mashambulizi ya aina hii.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW