1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kambi ya upinzani huenda ikaungana dhidi ya Mugabe.

27 Machi 2008

Harare.

Kambi za wapinzani nchini Zimbabwe zinaweza kuunda muungano dhidi ya rais Robert Mugabe iwapo uchaguzi mwishoni mwa juma hili utalazimisha kwenda katika duru ya pili.

Mugabe anakabiliwa na changamoto ya hali ya juu kabisa kutoka kwa mshirika wake wa zamani Simba Makoni pamoja na hasimu wake mkubwa Morgan Tsvangirai.

Licha ya upungufu mkubwa wa chakula na petroli Mugabe amesema kuwa anaimani kubwa ya kushinda uchaguzi huo.

Wagombea wa upinzani wameeleza wasi wasi wao kuwa uchaguzi wa Jumamosi utafanyiwa hila.