1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kambi ya Uturuki yashambuliwa kwa maroketi Iraq

1 Februari 2023

Washambuliaji ambao hawajatambuliwa leo wamefyatua roketi nane kwenye kambi ya kijeshi ya Uturuki iliyoko kaskazini mwa Iraq.

Symbolbild I Polizei in Karachi Pakistan
Picha: Rizwan Tabassum/AFP/Getty Images

Shirika moja la usalama la Iraq limesema hayo na kuongeza kuwa roketi mbili zilianguka ndani ya kambi hiyo ya kupambana na ugaidi.

Uturki imethibitisha shambulizi hilo na kuapa kulipiza kisasi. 

Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar amewaambia waandishi wa habari mjini Ankara kuwa mara kwa mara mashambulizi hufanywa dhidi ya kambi za Uturuki na ipo haja ya kuchukua hatua madhubuti.

Hakuna kundi ambalo lilikiri kuhusika na shambulizi hilo moja kwa moja punde lilipofanyika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW