1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Kambi ya wakimbizi Myanmar yashambuliwa kwa kombora

11 Oktoba 2023

Karibu watu 29 wakiwemo wanawake na watoto wameuwawa nchini Myanmar katika shambulizi lililofanywa katika kambi ya wakimbizi karibu na mpaka wa China.

Maziko ya waathirika wa shambulio katika kambi ya wakimbizi Myanmar
Maziko ya waathirika wa shambulio katika kambi ya wakimbizi MyanmarPicha: AFP

Duru zinaarifu kwamba utawala wa kijeshi wa Myanmar ndio uliofanya shambulizi hilo ambalo limelaaniwa na Marekani.

Msemaji wa jeshi Zaw Min Tun lakini amekanusha kuhusika kwake katika shambulizi hilo.

Duru hizo zinasema kombora liliipiga kambi ya wakimbiziwa ndani iliyoko kilomita 5 kutoka mji wa Laiza, iliko kambi ya kijeshi inayoendeshwa na Jeshi Huru la Kachin KIA, ambalo kwa miaka sasa limekuwa likizozana na jeshi la Myanmar.

Soma pia:Utawala wa kijeshi wa Myanamar na serikali ya Urusi wasaini mkataba wa ushirikiano kuhusu shughuli za uchaguzi

Hilo ni mojawapo ya mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kufanywa dhidi ya raia tangu jeshi lilipochukua madaraka katika mapinduzi ya mwaka 2021.