1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamisheni mpya ya EU inaanza kazi na mwelekeo mpya

1 Desemba 2024

Jopo jipya ya timu ya watendaji wakuu wa Umoja wa Ulaya, ikiongozwa na Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen imeanza kazi rasmi leo hii katika kipindi ambacho umoja huo ukikabiliwa changamoto mpya za kisiasa.

Ukraine, Kyjiw | Costa, Kallas und Kos besuchen als neue EU-Spitze ukrainische Hauptstadt
Rais mpya wa Baraza la EU António Costa, Mwakilishi mpya wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas na Kamishna mpya wa Marta Kos. 01.12,2024Picha: Ansgar Haase/dpa/picture alliance

Muistonia Kaja Kallas anakua na wajibu muhimu wa kuongoza safu ya ustawi wa diplomasia ya umoja, huku kambi hiyo ikijipanga kuanza kazi kwa Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump mapema mwakani. Kamisheni ya Umoja wa ya Ulaya ndiyo taasisi pekee iliyopewa mamlaka ya kupendekeza Sheria za Umoja wa Ulaya na kuhakikisha utiifu wa sheria katika mataifa wanachama. Kuanza kwa jukumu la kwanza la von der Leyen kama rais wa kamisheni 2019 kulikwenda sambamba na harakati za ulinzi wa mazingira duniani ambapo ilitoa muongozo wa kukabiliana ulinzi wake katika mataifa ya Umoja wa Ulaya uliofahamika kama "Mpango wa Kijani".

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW