1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampala. Jeshi laua waasi kumi wa LRA.

3 Oktoba 2005

Jeshi la Uganda limesema jana kuwa limewauwa waasi 10 wa jeshi la Lord Resistance Army LRA, katika mashambulizi mawili tofauti katika wilaya ya kaskazini ya Pader.

Msemaji wa jeshi katika eneo hilo kapteni Paddy Ankunda ameliambia shirika la habari la AFP kuwa jeshi la Uganda lilifanya mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya kundi la waasi wapatao 15 mapema jana Jumapili katika kijiji cha Lapul, kiasi cha kilometa 35 kaskazini mashariki ya mji wa Pader, na kuuwa waasi saba na kukamata baadhi ya vifaa vya kijeshi.

Waasi wengine watatu waliuwawa baadaye katika shambulio lingine katika kijiji cha Laguti, katika wilaya hiyo ya Pader.

Ankunda amesema kuwa jeshi halikupoteza askari kwa sababu mashambulizi yote yalikuwa ya kushtukiza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW