Kampala. Majeshi ya Uganda yashambulia waasi wa LRA,
6 Septemba 2005Matangazo
Majeshi ya serikali yakisaidiwa na helikopta yameshambulia maficho ya waasi kaskazini mwa Uganda , na kuwauwa waasi 12 na kulazimisha wengine kadha kukimbia msituni.
Msemaji wa jeshi la Uganda amesema leo kuwa , jeshi hilo halikupoteza mwanajeshi hata mmoja katika shambulio hilo dhidi ya waasi wa jeshi la Lord Resistance Army usiku wa Jumatatu.
Msemaji wa jeshi hilo Luteni Deo Akiki amesema jeshi la Uganda lilimkamata mke na mtoto wa miaka saba wa kamanda wa jeshi hilo la waasi katika shambulio hilo.Luteni Akiki amesema mke huyo wa kamanda wa jeshi la waasi anatibiwa kisaikolojia na anaweza kutoa taarifa zaidi juu ya waasi hao.