KAMPALA: Matumaini ya kupatikana amani Uganda
9 Novemba 2006Matangazo
Serikali ya Uganda imesema,inaamini mazungumzo ya amani pamoja na waasi wa kundi la LRA yatafanikiwa licha ya pande hizo mbili kutoaminiana na majadiliano hayo kucheleweshwa. Mwezi huu,pande hizo mbili zilirefusha makubaliano yanayotazamiwa kumaliza uasi wa miaka 20.Maelfu ya watu wameuawa katika vita hivyo na takriban watu milioni 2 wamepoteza makazi yao kaskazini mwa Uganda.