1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Mazungumzo kati na serikali ya LRA kuanza tena leo

7 Agosti 2006

Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Uganda na kundi la waasi la LRA yanatarajiwa kuanza tena hii leo mjini Juba nchini Sudan.

Msemaji wa ujumbe wa serikali ya Uganda, katika mazungumzo hayo, Paddy Ankunda, amesema wamepokea mwaliko kutoka kwa mpatanishi mkuu na kwamba wataondoka leo kwenda Juba. Ankunda amesema watajadili usitishwaji wa mapigano na kukomeshwa kwa ukatili.

Mazungumzo ya mjini Juba yanalenga kumaliza miaka ya vita kaskazini mwa Uganda ambavyo vimewaua maelfu ya watu na kuwalazimu wengine milioni mbili kuyahama makazi yao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW