KAMPALA : Museveni kuijenga upya kaskazini
16 Oktoba 2007Matangazo
Rais Yoweri Museveni wa Uganda hapo jana ameahidi kujenga upya eneo la kaskazini mwa nchi hiyo lililoathiriwa na vita kwa mpango wa msaada wa dola milioni 600 kwa ajili ya barabara, elimu na viwanda vidogo vidogo.
Museveni amewaambia wanadiplomasia, wafanya kazi wa misaada na wapiga debe wa amani mjini Kampala kwama lengo la mpango huo ni kuimarisha amani,kurudisha hali ya kawaida na ukarabati.
Mashirika ya misaada yanasema zaidi ya Waganda milioni moja bado wanaishi kwenye makambi machafu ya wakimbizi kaskazini mwa Uganda licha ya kuwepo kwa utulivu fulani tokea kusainiwa kwa usitishaji wa mapigano kati ya serikali na waasi wa LRA mwaka jana.