1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Waasi wa LRA wakataa msamaha wa serikali ya Uganda

7 Julai 2006


Waasi wanaopigana na serikali ya Uganda wamekataa msamaha uliotolewa na serikali hiyo,siku chache kabla ya mazungumzo ya kuleta amani kuanza.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda aliahidi kutoa msamaha huo kwa kiongozi wa waasi hao Joseph Koni ikiwa atakuwa ameacha harakati za kigaidi hadi kufikia mwisho wa mwezi huu.

Lakini msemaji wa kundi hilo la Lord’s resistance army ameeleza kuwa msamaha huo hauna maana yoyote,kwa sababu washiriki wote kwenye mazungumzo ya kuleta amani wanapaswa kuwa sawa.

Kiongozi wa kundi hilo Joseph Koni na makamanda wake wameshashtakiwa na mahakama ya kimataifa kwa kutenda uhalifu wa kivita.

Kutokana na vita baina ya waasi hao na serikali ya Uganda maalfu ya watu wameuawa na wengine milioni mbili wamelazimika kukimbia makwao

Mazungmzo baina ya waasi hao na serikali ya Uganda yalitarajiwa kuanza katika mji wa Juba kusini mwa Sudan chini ya usuluhishi wa serikali ya jimbo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW