1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Wajumbe kuishawishi mahakama ya The Hague isichukue hatua.

17 Machi 2005

Ujumbe kutoka kaskazini mwa Uganda umekwenda Uholanzi katika mahakama ya jinai The Hague kuishawishi mahakama hiyo isitoe agizo la kukamatwa na kufikishwa mbele ya mahakama hiyo viongozi wa waasi wa Lords Ressistance Army.

Wajumbe hao watakutana na kiongozi wa mashtaka wa mahakama ya jinai Moreno Ocampo ili kuwasilisha mapendekezo yao.

Wanasema kuwa hatua hiyo inaweza kuwasha moto wa mashambulizi mapya na kuvuruga juhudi za serikali ya Uganda za kuwashawishi waasi kusimamisha mapigano kaskazini mwa Uganda.

Zaidi ya watu milioni moja na nusu wamepoteza makao yao katika vita vya miaka 19 iliyopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW