1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampala. Wakimbizi wayakimbia makambi kutokana na vita pamoja na njaa.

14 Mei 2005

Shirika la umoja wa mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR, limesema kuwa kiasi cha wakimbizi 5,000 wamekimbia kutoka kusini mwa Sudan na kwenda kaskazini mwa Uganda tangu mwanzoni mwa mwaka huu kutokana na mashambulizi ya jeshi la waasi la Lord Resistance Army LRA.

Msemaji wa shirika hilo la kuwahudumia wakimbizi Roberta Russo ameliambia shirika la habari la AFP jana kuwa wakimbizi hao , ambao walianza kuwasili Januari, wamekaa sasa katika eneo kaskazini magharibi ya Uganda.

Wakimbizi hao wamesema kuwa wanakimbia mashambulizi ya LRA, wakati kiasi cha asilimia 50 ya wakimbizi hao wamekimbia makambi yao huko Nimule kusini mwa Sudan na kwenda Arua nchini Uganda kutokana na ukosefu wa chakula kwa kuwa chakula cha misaada kilikuwa hakipelekwi tena kwa muda mrefu sasa. Ameongeza kuwa wengi wa wakimbizi hao wanachunguzwa katika wilaya za mpakani za Uganda za Adjumani, Arua na Moyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW