1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Hali ya wasiwasi kwenye kambi ya wakimbizi wanyaruanda ya Nakivale

17 Septemba 2005

Wanajeshi na wafanyikazi wa mashirika ya kutoa misaada wamesema hii leo kwamba watu waliokuwa na mapanga wameteketeza makaazi kwenye kambi inayokaliwa na wakimbizi wa Kinyaruanda nchini Uganda.

Familia takriban 250 zimeachwa bila maskani baada ya nyumaba zao kuharibiwa kwenye hiyo ya Nakivale inayohudumia watu kiasi cha elfu 10 wengi wao wakiwa wahutu waliokimbia mauaji ya halaiki ya mwaka 1994.

Hali ya taharuki imetanda katika eneo hilo huku baadhi ya wakimbizi na wenyeji wakinyoosheana vidole vya lawama kwa madai ya kunyakuliana ardhi.

Msemaji wa jeshi la Uganda luteni kanali Shaban Bantariza amesema majeshi yamepelekwa katika kabi hiyo iliyoko kusini magharibi mwa Uganda kulinda amani katika eneo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW