KAMPALA:Jeshi la Uganda ladhibiti usalama mpakani na DRC
23 Agosti 2007Matangazo
Msemaji wa kikosi cha jeshi katika eneo la kusini magharibi mwa Uganda Tabaro Kiconco amesema kwamba kikosi chake kinadhibiti hali ya usalama katika eneo la mpaka wake na nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kutokana na hali mbaya ya usalama iliyosababisha takriban raia elfu kumi wa nchi hiyo jirani kutoroka siku ya jumanne na kuvuka mpaka kuingia nchini Uganda.
Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia wakimbizi hata hivyo limesema wakimbizi 8,500 walirejea nchini mwao Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo siku ya pili yake huku wakimbizi 1,500 wanawake na watoto wakiwa bado wameslaia nchini Uganda.