1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA.Serikali ya Uganda na waasi wa LRA watia saini mapatano ya amani

26 Agosti 2006

Serikali ya Uganda na waasi wa LRA wametia saini mkataba wa amani unaotrajiwa kumaliza mvutano baina ya pande hizo mbili.

Mpango huo umetiwa saini katika mji wa Juba nchini Sudan, unazitaka pande zote mbili kusimamisha mashambulio na propaganda za uadui kuanzia siku ya jumanne ijayo.

Mazungumzo ya kutafuta amani ya kudumu bado yataendelea hadi yatakapo kamilisha kusimamishwa kabisa mashambulio yaliyowauwa mamia ya watu na kuwafanya takriban watu milioni mbili kuyatoroka makaazi yao kaskazini mwa Uganda.

Waasi wa LRA walitangaza kusimamisha uadui dhidi ya serikali ya Uganda mano agosti 4.

Seriklali ya Uganda imetoa msamaha kwa viongozi wa LRA waliotakikana kufikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita na ambao wanajificha katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW