Kampeni kuanza mwisho wa mwezi lakini kuna changamoto
1 Novemba 2018Kampeni za uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimepangiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu, lakini bado tume ya uchaguzi inakabiliwa na changamoto kadhaa, zikiwemo uhamasishaji wa wananchi kuhusu uchaguzi kupitia mfumo wa elekroniki. Raia wengi nchini humo hasa kwenye maeneo ya vijijni hawaja wahi kutumia kompyuta.
Zikiwa zimesalia wiki tatu tu kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni za uchaguzi, hekaheka zimewakumba hasa wagombea kwenye uchaguzi wa ubunge wa taifa na ubunge wa majimbo ambao wameanza kujitayarisha kuhusu vifaa vya kampeni za uchaguzi. Garama kubwa kwa wagombea ni upatikanaji wa vifaa,wengi wamesafiri hadi Kinshasa au Kampala,Uganda na wengine hadi China.
Changamoto nyingine ni kwa tume huru ya uchaguzi ambayo imeandaa upigaji kura kwa matumizi ya mfumo wa elekroniki. Wengi miongoni mwa raia wa maeneo ya mashambani hawaja wahi kuona komputa. Wengine wakaazi wa Kindu tulio kutana nao,wamehoji umuhimu wa kuenda kupiga kura, wakielezea kusikitishwa na wabunge na viongozi waliochaguliwa kabla kutotekeleza ahadi zao.
Tume huru ya uchaguzi imetangaza kupokea nusu ya machines za kupigia kuras. Na ifikapo Novemba 10, vifaa vyote vya uchaguzi vitakuwa vimewasili nchini. Kwa jumla tume huru ya uchaguzi imepanga kutumia komputa laki moja kwa ajili ya upigaji kura wa desemba 23.
Mhariri: Iddi Ssessanga