1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni kwa ajili ya watoto nchini Guinea-Bissau

Lillian Urio15 Juni 2005

Guinea-Bissau, iliyo Magharibi mwa Afrika, ni mojawapo ya nchi 10 maskini kabisa duniani. Ili kuwasaidia watoto wa nchi hiyo, tarehe 15 mwezi huu, shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF na taasisi mbalimbali kutoka Gunie-Bissau, wataanzisha kampeni ya kulinda watoto.

Bendera ya Guinea-Bissau
Bendera ya Guinea-Bissau

Miaka 30 baada ya kupatata uhuru kutoka kwa Wareno, Guinea-Bissau hii bado haiko imara kisiasa, jambo ambalo ni muhimu katika kuisaidia uchumi kukua.

Tarehe 19 mwezi huu kutakuwa na uchaguzi wa rais nchini humo. Wagombea urais wamekubali kushirikiki katika kampeni hiyo ya kulinda watoto.

Kila mtu anataka kujumuika katika masuala ya watoto. Kutokana na maonio ya Yolanda Nunes Correia, mwakilishi wa UNICEF nchini humo, uchaguzi umeangua wakati mzuri. Wameweza kuwapata wagombea wa urais wote 13, kushiriki katika kampeni hiyo.

Lengo kuu la kampeni ni kuboresha maisha ya watoto. Tatizo kubwa ni huduma za afya, magonjwa ya malaria na kifua kikuu yanasumbua. Vituo vya afya vinatakiwa kuinua hali ya afya ya nchi. Kwa mujibi wa Umoja wa Mataifa, vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ni 204 kati ya watoto 1000.

Haman takwimu za ugonjwa wa UKIMWI, katika nchi hii ya Afrika Magharibi. Hii ni kwa sababu ya hali ya wasiwasi ya kisiasa, inayozuia serikali kufanya kazi kikamilifu.

Miezi mitatu iliyopita, Rais wa zamani Kumba Yala, alijaribu, bila mafanikio, kupindua nchi na kurudi madarakni. Aliondolewa madarakani, kwa nguvu, miaka miwili iliyopita. Tangu Guinea ipate uhuru mwaka 1974, kumekuwa na matukio ya mapinduzi mengi yaliofanywa na jeshi.

Takriban miaka 15 iliyopita, mfumo wa vyama vyingi ulianzishwa. Lakini kutokuwepo utulivu ya kisiasa, sio tu mfumo wa demokrasia unaoshindwa, bali pia kukua kwa mfumo mzuri wa kiuchumi.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa tayari hatua ndogo zimeshaanza kuchukuliwa. Lakini bado kuna mengi yanaoyo takiwa kutekelezwa.

Bi. Nunes Correia amesema:

“Lengo moja kuu la kampeni hiyo ni kuwahusisha wagombea wa urais katika mazungumzo juu ya malengo ya mailenia. NI muhimu sana kuwa viongozi wa nchi wanajishughulisha katika sekta ya maendeleo. Pia tunahitaji kuwahusisha wale wanaotoa misaada ya kifedha. Ili nchi iweze kutimiza wajibu wake, na kuwa nchi inayostahili watoto kuishi.”

Bi. Nunes Correia pia anazungumzia juu ya masuala ambayo sio rahisi kuyajadili katika nchi hiyo.

“Tungependa kama wanasiasa wangekubali mabadiliko katika taratibu zinazohatarisha maisha. Mfano wangepiga marufuku ukeketaji wa watoto na wanawake. Na pia kusitisha mpango wa watoto kulitumikia jeshi. Hayo pia yako katika ajenda yetu.”

Tatizo lingine linaloipa UNICEF wasiwasi ni elimu kwa watoto. Asilimia 38 ya watu wa Guinea-Bisau hawajui kusoma wala kuandika. Ni lazima mpango wa malezi uanzishwe, ambao utasaidia watoto wa kike kupata elimu.

Baadaye ndio tutaona kama wanasiasa, wagombea Urais sasa hivi, wataendelea kuiunga mkono kampeni hii baada ya uchaguzi utakaofanyika tarehe 19, mwezi huu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW