1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni za mwisho mwisho uchaguzi Marekani

7 Novemba 2016

Wagombea wa urais wa Marekani Donald Trump wa Republican na Hillary Clinton wa Democratic, wamepambana vikali katika majimbo ambayo ni lazima wapate ushindi katika kampeni za mwisho mwisho zenye mgawanyiko wa kihistoria.

USA Wahlkampf um Präsidentschaft Kombi Anhänger Clinton / Trump
Picha: picture-alliance/AP Photo/R. D. Franklin/ G. Herbert

Zikiwa ni chini ya saa 48  kuelekea siku ya kupiga kura, haikuwa wazi kama Clinton ambaye ni mgombea wa democratic atafaidika katika uchaguzi huo kufuatia tangazo la jana la FBI ambalo linamuondolea makosa yoyote kuhusu matumizi ya anuani yake ya binafsi ya barua pepe

Umaarufu wa Clinton ulipingua baada ya mkurugenzi wa FBI James Comey kuanzisha upya uchunguzi unaolenga kutaka kufahamu kama Clinton alifichua siri za Serikali ya Marekani kwa kutumia anuani binafsi ya barua pepe wakati akiwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo.

Kura ya maoni imekuwa ikionyesha kuwa wagombea hao wanakaribiana, wakati ambao Trump pia alianza kurejea tena ulingoni baada ya kukabiliwa na shutuma ya udhalilishaji kingono.

Bilionea na mgombea wa Republican amejipatia umaarufu kati ya vuguvugu la mashinani la wapiga kura wanaume weupe, ametua katika eneo Sarasota jimbo la Florida leo na kupokelewa kwa shauku na umati wa wanaomuunga mkono, baada ya kuwepo hapo kwa muda mgombea huyo mwenye umri wa miaka 70 anategemewa kusaifiri kuelekea North Carolina,Pennyslavia,  na Hampshire kwa ajili ya mkutano wa hadhara kabla ya tukio la kuhitimisha kampeni kufanyika Michigan

Picha za wagombea wa urais Clinton na TrumpPicha: picture alliance/dpa/A. Filippov

Trump asema Clinton amevunja rekodi ya ufisadi

Katika jimbo la Virginia jana siku ya jumapili aliwahutubia wafuasi wake katika mkutano wa suiku wa manane kwa kumshambulia mpinzani wake, kwa kumtaja kuwa ni mgombea fisadi kuwahi kutafuta kiti cha urais wa Marekani

Clinton mwenye umri wa miaka 69 ana mikutano ambayo imepangwa kufanyika usiku wa maneno, mikutano ambayo pia itawajumuisha watu maarufu akiwemo rais Barack Obama, siku ya jana Clinton alikuwa na hali ya matumaini pamoja na ishara za kitisho cha Trump

"Nataka tuwe na mjadala endelevu katika kuifanya nchi yetu vile inavyoweza kuwa,ninaamini kuwa miaka bora ya marekani iko mbele yetu ikiwa wote tutatimiza wajibu wetu" alisema Clinton

Ulimwengu unaangalia kwa hamu Trump akitumia umaarufu wake wa televisheni kuwa ndio kitu kinachomsukuma kueleka katika wadhifa huo mkubwa kisiasa ulimwenguni

Trump kwa upande wake anasema anahitaji kufanya mabadiliko halisi katika serikali.

"Mabadiliko halisi yanamaanisha kurudisha imani kwa serikali , tutaanza na kuondokana na Hilary Clinton, sawa? huo utakuwa mwanzo mzuri kwa sababu Clinton kaoza kwa rushwa kati ya watu wote ambao wamewahi kugombea nafasi ya uraisi wa marekani

Matokeo ya kura za maoni yanampa Clinton ushindi mwembamba wa kitaifa wa pengo la kati ya asilimia 3 na 5, matokeo mengi yanaonyesha kinyang'anyiro kikali ambapo Trump ataibuka mshindi katika baadhi ya majimbo muhimu

Mwandishi: Celina Mwakabwale/AFP

Mhariri:Yusuf Saumu