1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Kampeni za uchaguzi mkuu wa Rwanda zafungua pazia

Sylvia Mwehozi
22 Juni 2024

Kampeni za uchaguzi wa urais wa Rwanda uliopangwa kufanyika Julai 15, zimezinduliwa leo nchini humo huku Rais Paul Kagame akitarajiwa kurefusha utawala wake wa mkono wa chuma wa miaka 24.

Wagombea urais Rwanda |  Philippe Mpayimana | Paul Kagame | Frank Habineza
Wagombea urais Rwanda kutoka kushoto Philippe Mpayimana, Paul Kagame na Frank Habineza.Picha: AFP

Wanyarwanda takribani milioni 9 wameandikshwa kushiriki uchaguzi huo wa urais ambao kwa mara ya kwanza utafanyika sambamba na ule wa bunge.

Rais Kagame anachuana na wapinzani wawili ambao pia waliwania nafasi hiyo katika uchaguzi uliopita wa 2017. Wapinzani hao ni Frank Habineza kutoka chama cha Democratic Green na mwandishi wa habari wa zamani Philippe Mpayimana, anayeshiriki kama mgombea binafsi.

Kagame mwenye umri wa miaka 66 anasifiwa kwa mageuzi ya kiuchumi ya Rwanda hasa baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 lakini anakosolewa kwa ukiukaji wa haki za binadamu na kubinya upinzani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW