1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni za uchaguzi Kongo zinakamilika rasmi leo

18 Desemba 2023

Kampeni za uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinakamilika rasmi leo Jumatatu wakati shirika la Human Rights Watch likitahadharisha kuwa ghasia zinazohusiana na uchaguzi zinatishia kuvuruga uchaguzi.

DR Kongo Kinshasa | Wauasi wa rais Felix Tshisekedi
Wafuasi wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi mjini KinshasaPicha: Justin Makangara/REUTERS

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetoa wito kwa mamlaka za Kongo kuchunguza haraka na bila upendeleo matukio ya vurugu yanayohusiana na uchaguzi na kuwashtaki waliohusika, bila ya kujali waliohusika wanaegemea upande gani wa kisiasa.

Mtafiti mkuu wa Human Rights Watch tawi la Kongo Thomas Fessy ameeleza kuwa, shirika hilo limeorodesha matukio kadhaa ya vurugu kote nchini humo kati ya wafuasi wa vyama hasimu vya kisiasa ambayo yamesababisha mashambulizi ya kulipa kisasi, unyanyasaji wa kingono na kifo cha mtu mmoja.

Inaelezwa kuwa zaidi ya watu milioni 1.5 hawataweza kushiriki zoezi la kupiga kura katika maeneo yenye mizozo, hasa katika jimbo la Kivu Kaskazini na jimbo la magharibi la Mai-Ndombe.

Pia mamilioni ya wakimbizi wa ndani pia huenda wasishiriki zoezi hilo.

Upinzani umeonyesha wasiwasi wao juu ya udanganyifu katika kura huku wakiishtumu serikali kwa kula njama na tume ya uchaguzi CENI na mahakama ya katiba, ambayo ndio msuluhishi wa mwisho wa migogoro ya uchaguzi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW