Kampuni ya magari ya VW na kesi ya ufisadi
6 Julai 2005Gazeti la Ujerumani la ‘Süddeutsche Zeitung’ liliripoti, kwa mujibu wa mfanyakazi wa VW, kwamba baraza la wakurugenzi wa kampuni hiyo waliliruhusu baraza la wafanyakazi, kwa miaka mingi, kufanya safari nyingi zenye garama za juu.
Baadhi ya safari hizo zilifikia Euro 30,000 na pia waliwagaramia makahaba. Nalo baraza la wafanyakazi lilikuwa likiunga mkono ajenda za baraza la wakurugenzi. Habari za matatizo ya kampuni ya VW zimekuwa zinachapishwa kwenye magazeti, kutokana na kampuni hiyo kujikuta ina kasheshe mara kwa mara.
Hadi tukio hili lilipofichuliwa, suala la ufisadi na VW lilikuwa likiambatana na jina la Jose Ignacio Lopez.
Bwana Lopez alitokea kampuni ya General Motors, ijulikanayo kama GM, ya Marekani na akahamia Ulaya. Alikuwa na sifa ya meneja asiye penda mzaha na anayeweza kupunguza matumizi ya kampuni.
Katika mwaka wa 1993 fununu zilianza kuzagaa kuhusu sifa yake nyingine. Kuna waliodaui kwamba Bwana Lopez aliiba siri za ndani za kampuni ya GM na kuhama nazo kwenda VW. Mwanasheria wa serikali wa mji wa Darmstadt, kwenye jimbo la Hessen, sehemu iliyopo kampuni ya VW, akaanza kufufatilia madai ya wizi huo wa siri za kampuni.
Mwaka mzima wa migogor ulifuata, hadi kwenye ngazi za kisheria. Mwenyekiti wa wakati huo wa VW aliamua kutatua tatizo hili kwa kuangalia upi ni uhusiano muhimu kwa VW.
Alisema kwamba wakati wa vita, mwisho lazima kuwepo na aliyeshindwa na mshindi. Yeye pamoja na washiriki wengine walikuwa na lengo la kuifanya VW iibuke mshindi.
Mwaka wa 1996 Bwana Lopez aliondoka kwenye kampuni ya VW. Mwaka uliofuatia makampuni ya VW na GM yakafikia mapatanao. VW ikakubali kulipa milioni 100 za dola za Kimarekani, pamoja na malipo ya Euro bilioni 1, katika kipindi cha mda mrefu.
Mwanasheria wa serikali wa mji wa Darmstadt akawakilisha ripoti yake mwaka moja baadaye. Lakini wakati huo huo, tukio lingine la VW likachapishwa kwenye gazeti. Lilikuwa linamhusu Gerhard Schroder, ambaye kwa wakati huo alikuwa Waziri Mkuu wa Jimbo la Lower Saxony.
Tukio hilo lilikuwa juu ya safari ya ndege kwenda mji wa Viena, nchini Austria, iliyosemekana kwamba ililipiwa na VW. Lakini Waziri Schroeder alikataa jambo hilo na kusema alijilipia safari hiyo mwenyewe.
Mwanzoni mwaka huu habari nyingine zilijitokeza ju ya VW na siasa za ndani za Ujerumani. Uchunguzi ulibaini kuwa wabunge wawili wa chama cha SPD, Ingolf Viereck na Hans-Hermann Wendhausen, walikuwa wakipokea malipo kutoka kampuni. Lakini cha kushangaza ni kwamba hapakuwa na rekodi ya wao kulitumikia kampuni hilo, jambo ambalo wabunge hao wote wawili walikana sio kweli.
Jambo hili lilijadiliwa na vyombo vya habari na wanasiasa nchini kwa mda mrefu. Baada ya uchunguzi wa serikali, wabunge hao waliamriwa kurudisha malipo hayo kwa kampuni ya VW, kwa ujumla Euro 766,000. Lakini wabunge hao walipinga.
Leo hii suala hilo bado linaendelea katika ngazi za kisheria. Lakini sasa hivi VW inabidi itatue matatizo mengine. Kwa miaka kadhaa sasa kampuni hiyo haijakuwa ikipata faida katika uuzaji wa magari, kama hapo awali. Masoko ya nchi za nje sio imara kama awali. Wanmameneja mpya, Wolfgang Bernhard, aliyekuwa wa kampuni ya magari ya Daimler-Chrystler.
Ilitegemewa atalisaidia kampuni hilo. Lakini kwanza itambidi ashughulikie tatizo hili jipya la ufisadi, ambalo hadi sasa ukweli wote wa mambo haujulikani.
Haid sasa kinachojulikana ni kwamba Bwana Volkert wa baraza la wafanyakazi wa VW amejiuzulu wiki iliyopita. Anahisiwa kuhusika na kesi hiyo ya ufisadi.