1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiDenmark

Kampuni ya meli ya Maersk kuikwepa njia ya Bahari ya Sham

5 Januari 2024

Kampuni ya meli ya Maersk imesema kuwa itatumia rasi ya tumaini jema nchini Afrika Kusini badala ya njia ya bahari ya Sham na mfereji wa Suez baada ya waasi wa Houthi kuzishambulia meli zake za biashara.

Moja ya meli kubwa za makontena ya kampuni ya Maersk
Meli za kampuni ya Maersk zimeshuhudia mfululizo wa mashambulizi kutoka waasi wa Houthi wa nchini Yemen zinapopita kwenye Bahari ya ShamPicha: Karim Sahib/AFP

Kampuni hiyo ya Denmark imechukua hatua hiyo ikitoa sababu za kiusalama.

Mnamo siku ya Jumanne, Maersk iliweka wazi kuwa haitotumia tena bahari ya Sham na mfereji wa Suez "mpaka hali itakapobadilika" baada ya meli ya Maersk Hangzhou iliyokuwa inatokea Singapore kushambuliwa.

Tangu Novemba 18 mwaka uliopita, meli 25 za kibiashara zinazofanya safari zake kusini mwa Bahari ya Sham na Ghuba ya Aden zimeshambuliwa.

Bahari ya Sham na mrereji wa Suez ni moja kati ya njia muhimu za biashara ya kusafirisha mafuta duniani.

Hii ni mara ya pili kwa kampuni ya Maersk kusitisha safari zake katika bahari ya Sham.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW