Kampuni ya umeme ya Ghana yalikatia umeme bunge
1 Machi 2024Matangazo
Tukio hilo la siku ya Alhamis (Februari 29) lilivuruga mjadala bungeni
Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni hiyo, William Boateng, alithibitishia shirika la habari la Reuters kuwa kampuni yake iliamua kukata umeme baada ya bunge kushindwa kutimiza ahadi ya kulipa deni lake.
Soma zaidi: Uchaguzi wa Ghana 2020 ni kushindwa kwa Demokrasia
Hata hivyo, umeme ulirudishwa muda mfupi baadaye baada ya bunge hilo kulipa dola milioni moja na kuahidi kulipa fedha nyingine haraka iwezekanavyo.