1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kanasela wa Ujerumani azindua kituo cha kuwafundisha wanajeshi wa kuhifadhi amani wa kiafrika katika mji mkuu wa Ghana Accra.

Manasseh Rukungu23 Januari 2004
Kansela wa Ujerumani, Gerhard Schröder, leo alimaliza ziara yake nchini Afrika ya Kusini na sasa yuko safarini kuelekea Ghana, kituo chake cha mwisho cha ziara katika nchi nne za Afrika. Katika mpango wake Kansela atafunguahii leo, kituo cha juhudi ya amani, ambacho kitapewa jina la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan.

Uzinduaji wa kituo hicho kikubwa kwenye mwambao wa mji mkuu wa Ghana Accra, utakuwa kazi rasmi ya mwisho ya Kansela wa Ujerumani katika ziara yake ya kutembelea nchi nne za Afrika, Ethiopia, Kenya, Afrika ya Kusini na Ghana. Kituo hicho ambacho kitapewa jina la katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Kofi Annan, ni cha kisasa kabisa kwani kinapambwa kwa teknolojia mpya kabisa, mitambo ya setelite, video na ukumbi mkubwa wa mikutano pamoja na mafunzo ya wanajeshi wa kutunza amani wa kiafrika.

Gharama za kukijenga kituo hicho, kwa sehemu kubwa inabebwa na Ujerumani, na kitakuwa na nafasi kwa wanafunzi-wanajeshi kati ya 500 na 800 kila mwaka. Cha mstari wa mbele kabisa ni kuwaelimisha wanajeshi wa jumuiya ya nchi za Afrika ya Magharibi, ECOWAS. Kuhusu kituo hicho, Kanali-Luteni na kiongozi wa kundi la ushauri la jeshi la Ujerumani katika Ghana, Klaus Eckart, anaeleza kwa fahari juu ya jukumu litakalokuwa likishikiliwa na kituo hicho, anaposema.

Kituo hiki kitakuwa hasa ni shule ya kuunga mkono hisia za ushirika kati ya wanajeshi wa jumuiya ya ECOWAS, za kuhifadhi amani katika eneo hilo, bila kutegemea msaada kutoka nje, kwa mfano kutoka Marekani, Umoja wa mataifa au pengineko. Kituo hiki kitayafungua macho yale mataifa yanayohisi kuwa na dhamana ya kutunza binafsi hatima yao, pia kwa nia ya kuipunguzia mzigo wa gharama Ujerumani. Mwishio wa kumnukulu Luteni-Kanali wa jeshi la Ujerumani.

Luteni Klaus Eckart, alishiriki binafsi katika ujenzi wa kituo hicho, na kile anachosubiri sasa pamoja na wenzi wake, ni kuwapokelea karibuni walimu wa kijeshi kutoka kote duniani, licha ya kutoka Ghana yenyewe pia walimu kutoka nchi kama Uingereza na Ufaransa, madola mawili ambayo yana maarifa ya tangu wakati wa enzi ya ukoloni. Madarasa ya kituo hicho bado ni matupu, lakini katika wiki mbili mwishoni mwa mwaka uliopita, waliweza kufundishwa humo wanajeshi na watumishi wa huduma za kijamii kutoka mataifa 17 ya kiafrika, hususan kutoka nchi zinazokabiliana na mizozo kama Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Sierra Leone au Liberia. Kuhusu masomo hayo Luteni-Kanali Eckaert anasema: Kozi ya kwanza kabisa iliyofanyika hapa, ilikuwa ni ya kujaribu kuwarejesha tena katika maisha ya kawaida ya kijamii, wanajeshi waliokuwa wakitumikia harakati za amani katika maeneo ya mizozo. Nia nyingine ilikuwa ni kujaribu kuwakutanisha wakongwe na wanajeshi-vijana wa kiafrika pindi kuwafungua macho kufahamu umuhimu wa kuhifadhi amani. Mwisho wa kumnukulu Kanali-Luteni Eckart.

Mshiriki mmojawapo wa kwanza alikuwa ni Quabene Ukubi Apia, ambaye kabla ya kuwa sasa ni mtumishi wa wizara ya nje ya Ghana, alikuwa hapo kabla ni wanajeshi. Anafurahi sana kwamba, kituo hicho kitakuwa ni mchango muhimu katika jitihada ya amani.

Apia ni mmojawapo miongoni mwa wale wanaojiandaa kuwatafutia mahali pa kuishi wakimbizi wa vita vya kimkoa kwa kupitia kituo hicho. Anajitolea katika maandalizi haya, pia kwa sababu yeye binafsi alikwishajikusanyia maarifa machungu alipokuwa akitumikia jeshi la kutunza amani. Apia alikuwa ni mmojawapo kati ya wale waliofanya upatanishi kati ya makundi yaliyokuwa yakihasimiana nchini Liberia katika mji mkuu wa Ghana Accra. Licha ya msaada wa kugharamia ujenzi wa kituo hicho, Ujerumani pia itachangia wataalamu wa kuwatolea mashauri walimu wa wanajeshi hao wa kuhifadhi amani wa kiafrika.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW