Kandanda kuchezwa kwa dakika 60?
19 Juni 2017Bodi ya Kimataifa ya Kandanda – IFAB inasema kuwa kama mpira utachezwa kwa dakika 30 katika kila kipindi yatakuwa ni mabadiliko makubwa kwa sheria za kandanda. Hayo tu ni miongoni mwa nakala ya mkakati wa miaka mitano wa mada za kujadiliwa na mapendekezo ikiwa na malengo matatu: kuongeza heshima, muda wa kucheza na mvuto wa mchezo.
Wakosaoji wanasema kuwa mabadiliko kama hayo hayatakuwa na umuhimu wowote kama sheria ya kupoteza muda haitaimarishwa. Mapendekezo mengine ni pamoja na kuweka saa kubwa katika uwanja ambayo italingana na ile ya refa mbali na sheria mpya itakayoruhusu mchezaji kujipigia mpira ama hata kutamba na mpira wakati anapopiga mpira wa adhabu
Mabadiliko yoyote huenda yakachukua miaka mingi ya majaribio kabla ya kuidhinishwa na majaribio yatakayosimamiwa na IFAB, bodi inayotathmini sheria za kandanda kila mwaka na inajumuisha maafisa kutoka FIFA na vyama vinne vya kandanda vya Uingereza.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters
Mhariri: Josephat Charo