1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita vya Mashariki ya Kati vimekuwa na gharama kubwa

Angela Mdungu
21 Oktoba 2024

Kando ya madhila na madhara makubwa kwa maisha ya binadamu, vita vya Israel dhidi ya Hezbollah na wanamgambo wa Hamas vimekuwa na gharama kubwa, hali inayoibua wasiwasi kuhusu athari za vita hivyo kwa uchumi wa Israel.

Watu wa Gaza wakikimbia vita
Watu wa Gaza wakikimbia vitaPicha: Mahmoud Issa/PIN/IMAGO

Matumizi ya jeshi yameongezeka mara dufu, ukuaji wa uchumi umekwama hasa katika maeneo hatari ya mpakani ambako wakaazi wake walihamishwa. Wachumi wanasema huenda Israel ikakabiliwa na kudorora kwa uwekezaji pamoja wakati vita  ikiharibu bajeti na kuilazimisha kufanya maamuzi magumu kati ya masuala ya kijamii na jeshi.

Soma: Viongozi wa Umoja wa Ulaya na Ghuba wakutana katikati ya vita vya Gaza na Ukraine

Kutokana na vita, serikali inatumia fedha zaidi kwa ajili ya jeshi kutoka dola za Kimarekani bilioni 1.8 zilizotumiwa kabla ya shambulio la Hamas la Oktoba 7 mwaka 2023, hadi karibu dola bilioni 4.7 kufikia mwishoni mwa mwaka. Takwimu hizo ni kulingana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya mjini Stocholm.Uchambuzi: Mambo gani yamo kwenye mkakati wa Iran, Israel?

Taasisi hiyo inabainisha kuwa serikali ya Israel ilitumia dola bilioni 27.5 mwaka jna kwa ajili ya jeshi na kuifanya kushika nafasi ya 15 duniani ikiwa nyuma ya Poland. lakini imezipiku Canada na Uhispania ambazo zina idadi kubwa ya watu.

Watoto waliokimbia makazi Ukanda wa GazaPicha: Mahmoud Issa/Middle East Images/picture alliance

Vita hivyo vimeathiri ukuaji na upatikanaji wa nguvu kazi. Miezi mitatu baada ya Hamas kuishambulia Israel, uchumi wa Israel uliporomoka kwa asilimia 5.6 kiwango ambacho ni kibaya kabisa kwa nchi yoyote kati ya 38 za Jumuiya ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo ya OECD, kundi ambalo wengi wa wanachama wake ni mataifa tajiri.

Soma kwa kina: Mashambulizi ya Israel yawaua Wapalestina 11, Gaza City

Vita dhidi ya Hamas na Hezbollah vimekuwa na athari mbaya zaidi kwa uchumi wa Gaza ambao tayari ulikuwa umeporomoka, Asilimia 90 ya wakaazi wa ukanda huo wamelazimika kuyahama makazi yao na wengi wao hawana ajira.  Uchumi katika Ukingo wa magharibi pia umeathiriwa pakubwa. Maelfu ya Wafanyakazi wa Kipalestina walipoteza kazi zao baada ya Oktoba 7. Benki ya dunia inasema uchumi wa Ukingo wa Magharibi uliporomoka kwa asilimia 25 katika robo ya kwanza ya mwaka.Israel yaanzisha uvamizi mpya kaskazini mwa Gaza

Hofu ya kiusalama inakwamisha uwekezaji na kutibuliwa kwa safari za ndege hali inayozuia watu kusafiri na kusababisha sekta ya utalii itetereke. Wakati huohuo, serikali inalipia gharama ya makazi kwa ajili ya kuwahifadhi maelfu ya watu waliolazimika kuhama makwao katika eneo la kusini la mpaka wa Israel na Gaza na raia wa kaskazini waliokuwa hatarini kutokana na mashambulizi ya Hezbollah.

Jengo la ghorofa la Ahmed Al-Khatib lililoharibiwa katika shambulizi la mjini BeirutPicha: Louisa Gouliamaki/REUTERS

Hata hivyo, uchumi wa Israel bado una nguvu, hauonekani kuporomoka na ina deni la wastani. Taifa hilo lina uchumi mkubwa unaotegemea vyanzo vingi huku likiwa na sekta ya TEHAMA yenye nguvu inayosaidia mapato ya kodi na matumizi ya ulinzi.

Pamoja na hayo, bajeti ya Waziri wa fedha Bezalel Smotrich kwa mwaka 2025 inatabiri upungufu wa asilimia nne. Kwa upande wake taasisi ya utafiti wa uchumi ya Moody's inatazamia kuwa Israel itakuwa na upungufu wa asilimia 6 katika bajeti yake mwakani.

Mashambulizi ya Israel yawaua watu 40 Gaza

Marekani ambayo ni mshirika mkuwa wa Israel imeongeza msaada wa kijeshi kwa nchi hiyo. Kabla ya vita ilikuwa ikiipatia Israel bilioni 3.8 kila mwaka, lakini tangu kuanza kwa vita Ukanda wa Gaza, Marekani imeshatumia kiasi kisichopungua dola bilioni 17.9. Kando ya msaada huo wa kijeshi baraza la wawakilishi la Marekani mwaka  2023, lilipitisha mkopo wa dola bilioni 9 unaoiruhusu Israel kurejesha kwa riba nafuu.Mzozo wa Mashariki ya Kati wagubika mkutano wa viongozi wa EU na Ghuba

Kama hatua za kunusuru uchumi, serikali ya Israel imeunda tume ya kujadili msaada wa Marekani wa hivi karibuni zaidi chini ya aliyekuwa kaimu mshauri wa usalama wa taifa Jacob Nagelili ili itoe mapendekezo kuhusu ukubwa wa bajeti ya ulinzi na namna ongezeko la matumizi ya ulinzi yanavyoweza kuathiri uchumi.