Kane atupia mawili Bayern ikiicharaza Cologne 4-1
30 Oktoba 2025
Matangazo
Klabu ya kandanda ya Bayern Munich usiku wa kuamkia leo imeicharazaFC Köln magoli 4-1 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Ujerumani DFB-Pokal.
Katika mchezo huo, nahodha wa England, Harry Kane alitupia wavuni magoli mawili na kufikisha jumla ya magoli 22 katika michezo 14 pekee aliyocheza msimu huu. Kocha wa Bayern Munich Vincent Kompany ametoa pongezi kwa timu yake ambayo pamoja na ushindi huo imeweka rekodi ya kuwa timu pekee katika ligi tano bora barani Ulaya kushinda mechi zote 14 za msimu huu.
Katika mchezo mwingine wa DFB-Pokal, Bayer Leverkusen walilazimika kupata ushindi wa 4.2 dhidi ya Paderborn baada ya dakika 120, Mainz 05 wakiwa nyumbani wamecharazwa na Stuttgart magoli 2-0.