1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kane: England haina mgawanyiko kambini

14 Julai 2026

Nahodha wa timu ya England Harry Kane amekanusha, juu ya taarifa za kuwepo kwa mgawanyiko ndani ya kikosi hicho kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina siku ya Jumatano.

Kombe la Dunia  2026 | England | Nahodha Harry Kane
Nahodha wa timu ya England Harry KanePicha: Moritz Müller/IMAGO

Kauli hiyo imekuja baada ya kiungo Jude Bellingham kuonekana kutofautiana na tathmini ya kocha kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Norway katika muda wa nyongeza.

Baada ya mechi hiyo iliyochezwa katika joto kali mjini Miami nchini Marekani, Bellingham alisema si rahisi kuelewa mazingira hayo kwa mtu ambaye hajayakabili uwanjani, akionekana kujibu kauli ya Tuchel kwamba England haikucheza vizuri.

Hata hivyo, Kane amesema tofauti hizo za maoni hazimaanishi kuwa kuna mzozo kambini.

“Ni rahisi kujaribu kuunda picha ya mgawanyiko, lakini ukweli ni kinyume chake. Tumefika hapa kutokana na umoja wetu,” alisema Kane.

Nahodha huyo alifafanua kuwa Bellingham alikuwa ametoka tu kumaliza mechi ngumu alipoulizwa kuhusu kauli za kocha.

Kane: Tuchel ni miongoni mwa Kocha bora

Kane amemtetea Tuchel akisema uwazi wake wa kuzungumza na kutoa tathmini za moja kwa moja ni moja ya sifa zinazomfanya kuwa miongoni mwa makocha bora duniani.

Kocha wa kikosi cha England Thomas Tuchel Picha: Javier Garcia/Shutterstock/IMAGO

“Anasema anachokiamini na wachezaji tunamwelewa." Alisema na kuongeza kuwa amekuwa akiisifu timu mara nyingi kwa kiwango chake cha kujituma na kupambana,” alisema.

Englandsasa inajiandaa kuivaa Argentina katika nusu fainali, huku Kane akisisitiza kuwa mshikamano wa kikosi utaendelea kuwa silaha muhimu katika harakati za kutinga fainali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW