Kane kuikosa mechi ya Gladbach
6 Machi 2026
Lakini kocha Vincent Kompany anatarajia Muingereza huyo arudi katika mechi yao ya Ligi ya Vilabu Bingwa wiki ijayo.
Kompany amesema Kane ambaye ndiye mfungajibora ataikosa mechi hiyo dhidi ya Borussia Mönchengladbach kutokana na jeraha dogo la msuli.
"Harry Kane hatopatikana. Aligongwa kidogo kwenye msuli wa mguu na hajapona bado, ni kugongwa tu, si kitu kikubwa kwa sasa, tutahitaji kama siku moja zaidi ili weze kuwa sawa na kucheza."
Koampany lakini amesema hatarajii Kane aikose mechi ya Jumanne ya Ligi ya Vilabu Bingwa hatua ya 16 bora nchini Italia dhidi ya Atalanta.
Kane ambaye hajaanza mechi zote za Bundesliga msimu huu ana jumla ya mabao 30 katika ligi hiyo ya Ujerumani na amefunga magoli 8 katika mechi 4 zilizopita za Bundesliga.
Anaifukuza rekodi ya Robert Lewandowski ya msimu wa mwaka 2020/2021 ambapo alifunga mabao 41 ya Bundesliga msimu huo.