1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kanisa kama msuluhishi

13 Januari 2015

Chini ya wiki moja tangu pale Wasri Lanka walipomchagua rais mpya Sirisena Papa Francis amewasili katika nchi hiyo yenye waumini wengi wa Kibudha jana Jumanne(13.01.2015),akianza ziara ya wiki nzima.

vor dem Papstbesuch auf den Philippinen
Papa Francis akiwa Sri LankaPicha: Getty Images/Dondi Tawatao

Katika wakati wa kampeni ya uchaguzi nchini Sri Lanka , jamii ya waumini wa Kikristo nchini humo ilivutiwa na wagombea wote rais wa zamani Mahinda Rajapaksa na mrithi wake Maithripala Sirisena. Wadadi wanasema kanisa Katoliki linaweza kuwa daraja la kuleta ukaribiano kati ya jamii hasimu za Wasinhale ambao ndio wengi na Watamil .

Waumini wakimpokea papa Francis Sri LankaPicha: Munir Uz Zaman/AFP/Getty Images

Wakati wote ambapo mbio za kuelekea uchaguzi zilivyokaribia, wagombea hao wawili walipambana kuweza kupata kura za Wakristo. Mwezi Novemba mwaka 2014, wafuasi wa Rajapaksa waliweka mabango kote nchini yakionesha kiongozi wao akiwa na papa Francis. Rajapaksa na Sirisena pia walihudhuria mkutano wa maaskofu wa Kikatoliki mapema mwezi Desemba kuonesha kuunga kwao mkono Wakristo.

Lakini kundi la Wakatoliki halina nia ya kuhusishwa na kambi zote mbili. Pia wameonya kuhusu mgawanyiko katika ziara ya papa Francis, iliyokuwa ianze kuanzia jana Januari 13 hadi 15.

Polisi wakilinda usalama wakati wa ziara ya papa FrancisPicha: L. Wanniarachchi/AFP/Getty Images

Rajapaksa achafuliwa

Mwaka mmoja uliopita , mkutano wa maaskofu ulitoa ushahidi wa kuchafua dhidi ya sera za Rajapaksa ambazo alizitumia baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyochukua miongo kadhaa. Desemba mwaka 2013, mkutano huo ulitoa wito wa maridhiano na ujenzi mpya wa taifa hilo, "mageuzi ya msingi" na kurejea katika kile ilichokiita "utawala wa sheria".

Kuanzia mwaka 1983 hadi 2009, wapiganaji wa Kitamil walitaka kujitenga walipigana kupata uhuru wa eneo lao katika upande wa kaskazini na mashariki mwa nchi hiyo. Mzozo huo wa kijeshi ulimalizika kwa kushindwa kwa waasi , na kusababisha kiasi ya watu 80,000 ahadi laki moja kupoteza maisha.

Wakristo Wakatoliki ni asilimia sita ya wakaazi wote wa Sri Lanka wapatao milioni 21. Wakatoliki wanapatikana kutoka jamii zote za Wasinhale waliowengi na Watamil ambao ni wachache.

Kanisa Katoliki linaweza kuchukua jukumu muhimu katika wakati huu na pia kutokana na ukweli kwamba ni taasisi pekee yenye ushawishi ambayo inawawakilishi katika jamii zote.

Papa anatafuta amani

Kanisa la Sri Lanka limeweka wazi kwamba papa anatafuta amani," mwanasayansi ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Heidelberg na mtaalamu wa masuala ya Sri Lanka Radu Carciumaru amesema.

Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa FrancisPicha: B. Weerasinghe/Getty Images

"Anakuja kukutana na Wasri Lanka , ambao ni Wasinhale, Watamil, Wabudha na Waislamu. "Ni tukio la kiroho,"ameongeza.

Lakini miaka mitano baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, hali ya kisiasa katika taifa hilo la visiwani inaendelea kuwa ya wasi wasi.

"Bado kuna hali ya juu ya kutoaminiana katika maeneo ya zamani ya vita , hususan katika eneo la kaskazini lenye shughuli nyingi za kijeshi. Hali hii inafanya kutokuwa na uwezekano wa kurejea katika maisha ya kawaida, amesema Carciumaru, akiongeza kwamba serikali iliyopita haikufanya lolote kubadilisha hali hiyo. " Mtu anaweza hata kusema serikali ya Rajapaksa imezuwia juhudi za uchunguzi wa uhalifu wa kivita uliofanywa na jeshi lake. Wakati huo huo, mamia ya wapiganaji waasi wa Kitamil wa zamani bado wanaendelea kubaki magerezani.

Papa Francis anatarajiwa kutoa wito tena na tena wa amani, hususan wakati mzozo huo wa kikabila kati ya Wasinhale walio wengi na Watamil ambao ni wachache sio suala pekee linalowatenganisha kijamii watu wa nchi hiyo. Wabudha wenye msimamo mkali wanachochea ghasia na kuchokoza makundi mengine ya kidini, hususan Waislamu pamoja na Wakristo wa madhehebu ya kiinjili ambao inawashutumu kwa kufanya kazi za kimisionari, amesema Carciumaru.

Papa Francis akiwa na rais mpya wa Sri Lanka SirisenaPicha: Reuters/S. Rellandini

nafikiri Sri Lanka bado iko mbali mno na kupata mtazamo wa pamoja. lakini hapa ndio kanisa Katoliki linalokuwa muhimu. Hii ni mifano kadhaa ya vipi juhudi zinazoelekezwa na kanisa zinavyoonekana, hususan katika ngazi hii. Pamoja na hayo , kanisa linaunga mkono kwa dhati elimu na linahusika katika kazi za hisani , ambazo zote zinasaidia kuimarisha jamii ya Sri Lanka. Ziara ya Papa Francis itasaidia kuonesha juhudi hizi zote.

Mwandishi: Thomas Latschan / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman