1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVatican

Papa Leo atoa wito wa kufanikisha mpango wa amani huko Gaza

5 Oktoba 2025

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo amesema ana matarajio kuwa mpango wa hivi karibuni wa kumaliza vita huko Gaza utapata matokeo yanayotarajiwa.

Vatikan | Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIVPicha: Filippo Monteforte/AFP

Akizungumza wakati wa sala ya kila wiki, Papa amezitaka pande zote kushiriki kikamilifu katika mchakato wa amani, akisisitiza hitaji la haraka la kuumaliza mzozo huo na kuanzisha "amani ya haki na ya kudumu".

Wapatanishi wa Israel na Hamas wamekutana Jumapili mjini Cairo katika mazungumzo ya kujaribu kumaliza mzozo huo wa  Mashariki ya Kati.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amesema Israel na Hamas zimekubaliana kuhusu sehemu kubwa ya mpango huo wa amani uliopendekezwa na rais Donald Trump lakini akasisitiza kuwa suala la kundi hilo kupokonywa silaha ndio linalojadiliwa kwa sasa na linatarajiwa kuleta utata.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW