1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Friedrich Merz aanza ziara rasmi nchini India

Josephat Charo
12 Januari 2026

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amewasili India leo Jumatatu kwa ziara rasmi ya siku mbili kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.

Kansela Friedrich Merz wa Ujerumani amewasili nchini India kwa ziara rasmi ya siku mbili.
Kansela Friedrich Merz wa Ujerumani amewasili nchini India kwa ziara rasmi ya siku mbili.Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Wizara ya mambo ya nje ya India imesema katika taarifa kuhusu ziara ya kansela Friedrich Merz kwamba yeye na mwenyeji wake Narendra Modi watazingatia maendeleo yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali za ushirikiano wa kimkakati wa India na Ujerumani, ambao ulikamilisha miaka 25 mwaka jana.

Merz na Modi watajadili kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, uwekezaji, teknolojia, elimu na ulinzi.

Kansela Merz pia anatarajiwa kutembelea Gandhi Ashram, ambayo hapo awali yalikuwa makazi ya Mahatma Gandhi na kitovu kikuu cha mapambano ya India ya uhuru kutoka kwa utawala wa kikoloni wa Uingereza.

Siku ya Jumanne, Merz atatembelea Bengaluru, kitovu cha tasnia ya teknolojia ya hali ya juu ya India.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW