1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Merkel arejea nyumbani toka Warsaw

18 Machi 2007

Berlin:

Kansela Angela Merkel amerejea nyumbani mjini Berlin baada ya ziara ya siku mbili mjini Warsaw.Msemaji wa ofisi ya kansela amesema Poland imekubali kushirikiana kwa dhati na Ujerumani katika juhudi za kuupatia ufumbuzi mzozo uliosababishwa na kukwama katiba ya Umoja wa ulaya.Hapo awali rais Lech KaCZYNSKI wa Poland aliwaambia maripota mjini Warsaw,huenda akatia saini “muongozo wa Berlin” hata kama hajaridhika moja kwa moja na maandishi yake.”Muongozo huo wa Berlin ni sehemu ya juhudi za kansela Angela Merkel za kufufua mazungumzo kuhusu katiba ya Umoja wa ulaya.Katiba hiyo imekwama tangu ilipokataliwa katika kura ya maoni nchini Ufaransa na Uholanzi miaka miwili iliyopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW