1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Merz aelekea Jordan na Israel

6 Desemba 2025

Kansela Friedrich Merz wa Ujerumani Friedrich Merz kaanza safari kuekea Israel na Jordan, baada ya mazungumzo kwa njia ya simu na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas.

Marekani Washington 2025 | Kansela Friedrich Merz baada ya kukutana na Trump na Zelenskyy
Kansela Friedrich Merz baada ya kukutana na Trump na Zelenskyy - 18.08.2025Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Kiongozi huyo wa Ujerumani ataanzia ziara yake mjini Amman, ambako amepangwa kukutana na Mfalme Abdullah II wa Jordan. Baadaye leo hii atapokelewa na Rais wa Israel Isaac Herzog mjini Jerusalem. Ingawa mazungumzo na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu yamepangwa kufanyika kesho Jumapili.Merz pia atatembelea Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari ya Wayahudi (Yad Vashem) ili kuweka shada la maua, jambo ambalo ni desturi ya kila ziara ya kwanza ya kansela wa Ujerumani nchini Israel.Ziara hiyo inatarajiwa kujikita katika kurekebisha uhusiano uliokuwa na mvutano kati ya nchi hizo mbili na kuimarisha zaidi usitishaji wa mapigano huko Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW