1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz awasili China kwa mazungumzo ya biashara na usalama

25 Februari 2026

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz ameanza ziara yake ya siku mbili nchini China Jumatano 25.02.2026 anakotarajiwa kujikita katika mazungumzo yatakayogusa maeneo kadhaa yakiwemo biashara na ulinzi.

 Ziara ya Friedrich Merz nchini China 25.06.2026
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz akiwa na Waziri Mkuu wa China Li Quiang mara baada ya kuwasili ChinaPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa China Li Qiang mara baada ya kuwasili Beijing, Merz amesema anazingatia umuhimu mkubwa katika kuimarisha zaidi ushirikiano kkadri iwezekanavyo.

Ziara ya kwanza China tangu Merz alipoingia madarakani

Ziara hii ni ya kwanza ya Merz katika taifa hilo ambalo ni mshirika mkubwa wa kibiashara kwa Ujerumani. China pia ni mshindani mkubwa wa kiteknolojia kwa Ujerumani iliyo na uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya.

Katika mazungumzo yake atakayofanya na Rais Xi Jinping, Merz anatarajiwa kutilia mkazo maslahi ya Ujerumani na Ulaya, ikiwemo  kuongeza shinikizo kwa Urusi kumaliza vita nchini Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW