1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Merz wa Ujerumani yuko ziarani Italia leo

17 Mei 2025

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni anatarajiwa hivi leo kumpokea Kansela mpya wa Ujerumani Friedrich Merz mjini Roma, hii ikiwa ni ziara ya kwanza ya Merz nchini Italia tangu alipoingia madarakani.

Italia I Ujerumani
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz akiwa na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia MeloniPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni anatarajiwa hivi leo kumpokea Kansela mpya wa Ujerumani Friedrich Merzmjini Roma , hii ikiwa ni ziara ya kwanza ya Merz nchini Italia tangu alipoingia madarakani.

Viongozi hao wawili ambao tayari walikutana jana Ijumaa katika mkutano wa viongozi wakuu wa Ulaya huko Tirana, Albania watakutana kwa mazungumzo katika makazi rasmi ya waziri mkuu ya Palazzo Chigi.

Tangu alipoidhinishwa kuwa Kansela mpya wa Ujerumani, Merz tayari ameyatembelea mataifa ya Ufaransa, Uingereza, Poland na Ukraine lakini pia Ubelgiji alipokwenda katika mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya na ule wa nchi wanachama wa Jumuiya ya kujihami ya NATO.