1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Olaf Scholz aashiria uchaguzi wa mapema zaidi

11 Novemba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema yauko tayari kuitisha kura ya imani kwa bunge kabla ya sikukuu ya Krismasi.

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz asema inawezekana kura ya bunge ya imani ikafanyika mapema, kuliko alivyotaja awaliPicha: Carsten Koall/dpa/picture alliance

Matamshi yake yanaashiria muda wa mapema zaidi, tofauti na ule wa awali wa mwezi Januari, kufuatia kuongezeka kwa shinikizo kutoka kwa wanasiasa na umma la kufanyika uchaguzi wa mapema.

Scholz amesema, kwenye mahojiano na kituo cha utangazaji cha ARD kwamba kura hiyo inategemeana na makubaliano kati ya chama chake cha Social Democrat, SPD na upinzani kuhusiana na muda.

Ujerumani ilitumbukia kwenye sintofahamu ya kisiasa wiki iliyopita baada ya muungano wa serikali ya Scholz kuvunjika kufuatia mvutano juu ya kiwango cha fedha ambacho serikali inapaswa kukitumia kuimarisha uchumi na kuisaidia Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW