1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Olaf Scholz ahimiza kuachana na nishati ya mafuta

2 Desemba 2023

Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz lameutolea wito ulimwengu kuondosha kabisa matumizi ya makaa ya mawe, mafuta na gesi. Kansela huyo ameyazungumza hayo huko Dubai.

COP28 Climate Summit | Olaf Scholz
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani akiwa katika mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi Cop28 huko Dubai.Picha: AP/Rafiq Maqbool/picture alliance

Amewaambia wajumbe kutoka katika pande zote za ulimwengu kuwa lazima kuwepo na dhamira thabiti katika kutekeleza lengo hilo. Na kuongeza kuwa wote kwa pamoja wanaweza kuanzisha jitihada ya utekelezaji katika mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi.Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa Ujerumani, bado upo uwezekano wa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu inayoharibu mazingira katika muongo huu kwa chini ya kiwango cha nyuzi joto 1.5 katika viwango vya celsius kwa zingatio la mkataba wa Paris wa mwaka 2015.Kansela Scholzamesema sayansi inasema wazi kuwa jitihada hizo zinapaswa kuharakishwa, pamoja na kuwepo na mivutano ya kimataifa, akimaanisha vita katika Ukanda wa Gaza na Ukraine, ambayo pia ni mada kuu kwenye mkutano huo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW