1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Scholz akataa kutoa makombora ya Taurus kwa Ukraine

5 Oktoba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anapinga mpango wa kuipa Ukraine makombora aina ya Taurus, ya masafa ya kilometa 500, licha ya Ukraine kusisitiza maombi juu ya silaha hizo.

Bundeskanzler Scholz empfängt Nikolaj Denkow in Berlin
Picha: Political-Moments/IMAGO

Vyanzo vya serikali vimethibitisha msimamo huo wa Kansela Scholz kwa shirika la habari la Ujerumani, dpa. Hata hivyo Kansela wa Ujerumani yuko tayari kuliangalia tena suala hilo baadaye lakini kwa sasa amesema hatatoa kibali cha kuipa Ukraine makombora hayo.

Badala yake Ujerumani inakusudia kuweka mkazo juu ya kuipa Ukraine mizinga na makombora ya ulinzi wa anga. Kwa mujibu wa gazeti la Ujerumani, ”Bild” uamuzi wa Kansela Olaf Scholz  umeshawasilishwa kwa Ukraine.

Ukraine ilianza kutoa maombi juu ya makombora ya Ujerumani aina ya Taurus mnamo mwezi wa Mei. Ujerumani inahofia makombora hayo ya masafa ya kilometa 500 yanaweza kushambulia ndani ya Urusi.